Course Purpose
Madhumuni makuu ya kozi hii ni kuwawezesha walimu na wanafunzi kujipatia maarifa, stadi, mitazamo, na thamani muhimu zinazohusu matumizi na mafunzo bora ya lugha ya Kiswahili. Kozi hii inalenga kuimarisha uwezo wao wa kutumia mikakati yenye ufanisi katika kujifunza lugha, ikijumuisha stadi zote nne za msingi: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma, na Kuandika. Hii itawasaidia washiriki kukuza weledi wao wa lugha na uwezo wao wa kufundisha kwa tija, huku wakikabiliana na mazingira ya kisasa ya elimu.
Course Learning Outcomes
Ifikapo mwisho wa kozi hii, mwanafunzi anapaswa kuwa na uwezo wa:
Kusimulia historia ya ukuzaji na ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili katika shule za sekondari nchini Kenya.
Kuchunguza na kukuza stadi (ujuzi) zinazohitajika kwa ajili ya ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya pili nchini Kenya.
Kufasiri na kueleza yaliyomo katika silabasi/mtaala wa lugha ya Kiswahili kwa shule za sekondari.
Kuunda na kutumia zana za kupima stadi za lugha (Linguistics skills), vipimo vya majaribio, tathmini, na utoaji wa mrejesho (feedback).
Course Content
Kozi hii inalenga kukuza ujuzi wa lugha ya Kiswahili kwa kuwapa walimu na wanafunzi maarifa kuhusu umuhimu wa stadi zote nne za lugha: Kusikiliza, Kuongea, Kusoma, na Kuandika. Maudhui yatashughulikia uchunguzi wa lugha katika vyombo vya habari (magazeti), kurekebisha shida za matamshi kwa kutumia vifaa vya kisasa, na kuchambua mfumo wa elimu wa CBC kwa shule za sekondari. Washiriki watafundishwa stadi za utayarishaji wa hati za mafundisho (muhtasari wa ratiba na taarifa ya somo), kuimarisha utahiri katika kufundisha lugha, na kujifunza njia mbalimbali za kufundisha fasihi ya Kiswahili. Hatimaye, kozi itajumuisha uhariri na usahihishaji wa ujuzi wa lugha (sarufi na insha) kulingana na mahitaji ya kazi mbalimbali.
